ISRAEL Mwenda beki wa kupanda na kushuka sasa ni kijani na njano baada ya kutambulishwa rasmi ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sead Ramovic.
Nyota huyo alitambulishwa na Singida Black Stars msimu wa 2024/25 ambapo inatajwa kuwa dau lake ilikuwa ni milioni 15o lilimvuta akasaini mkataba ndani ya timu hiyo inayotumia Uwanja wa Liti.
Aliibuka hapo akitokea Simba ambapo huko mshindani wake wa namba alikuwa ni Legend, Shomari Kapombe ambaye bado yupo ndani ya kikosi cha Simba.
Yanga imemkaribisha kijana huyo ambaye atakuwa hapo kwa mkopo wenye kipegele cha kumnunua moja kwa moja ikiwa atafanya vizuri.
Kupitia ukurasa wa Instagram Yanga wameandika namna hii: “Karibu Jangwani Israel Mwenda.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.