WAWAKILISHI wa kimataifa Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukamilisha kazi ugenini kwa kupoteza kwenye mchezo uliochezwa Desemba 7 2024 Uwanja wa 5 July uliposoma MC Alger 2-0 Yanga wameanza safari ya kurejea Dar kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazofuata.
Kwenye mchezo huo mabao yote yalifungwa kipindi cha pili na Ayoub Abdellaoui dakika ya 64, Soufiane Bayazid dakika ya 90. Katika dakika 45 za mwanzo Yanga walicheza kwa kukaba kwa nguvu na kuziba njia za wapinzani wao.
Mchezo wa kwanza hatua ya makundi walipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan ambapo katika mchezo huu uliochezwa Uwanja wa Mkapa mabao yote mawili yalifungwa pia kipindi cha pili.
Tayari msafara wa wachezaji pamoja na viongozi umeanza safari kurejea Dar miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara huo ni Aziz Ki, Clement Mzize, Kennedy Musonda, Prince Dube.
SALAMU ZA PONGEZI KWA WAZIRI
Ikiwa ni muda mfupi baada ya taarifa kueleza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amehamisha majukumu ya sekta ya habari kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na kumteua Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yanga wametuma salamu za pongezi.
Taarifa ya uteuzi na mabadiliko ya viongozi, imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Sharifa Nyanga. Taarifa hiyo imeeleza kuwa uapisho wa viongozi walioteuliwa Desemba 8 2024 utafanyika Ikulu Ndogo, Zanzibar Desemba 10, 2024.
Kupitia Insta Yanga wameandika namna hii: “Hongera Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.) kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.