VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC wamebainisha kuwa baada ya kumaliza kazi ya kuvuna pointi tatu dhidi ya Dodoma Jiji, wanarejea Dar kwa usafiri wa treni ya mwendokasi , SGR Tanzania
Ikumbukwe kwamba Desemba Mosi 2024, Azam FC walikuwa ugenini kwenye msako wa pointi tatu dhidi ya Dodoma Jiji wakaibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Kwenye mchezo huo jumla mabao manne yalifungwa, mtupiaji wa kwanza ni Yannic Bangala ambaye alijifunga kwa upande wa Azam FC ilikuwa dakika ya 7 huku yale ya Azam FC yakifungwa na Nassor Saadun aliyekomba tuzo ya mchezaji bora wa mchezo, Feisal Salum kwa mkwaju wa penalti dakika ya 45 na Dickson Mhilu alijifunga dakika ya 60.
Azam FC ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 30 kibindoni baada ya kucheza mechi 13 wanafuatiwa na Simba nafasi ya pili pointi 28 baada ya kucheza mechi 11.
Kupitia kwenye ukurasa wa Instagram, Azam FC wameandika namna hii: ” Azam FC tumefurahia sana kusafiri kishua na treni hiyo ya viwango isiyochosha na yenye huduma bora kabisa ndani yake kwa wasafiri. Tunaipongeza sana Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais wetu mpendwa, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji huu mkubwa.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.