LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea kutimua vumbi ambapo leo Novemba 30 kuna mechi za funga Novemba 2024 kwa wababe kuwa uwanjani kusaka ushindi.
Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Sead Ramovic itakuwa ugenini kusaka pointi tatu dhidi ya Namungo, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa.
Ni saa 12:30 jioni, Namungo wataikaribisha Yanga kwenye mchezo huo wa ligi kwa wababe hao kusaka pointi tatu ndani ya dakika 90.
Ikumbukwe kwamba kwenye mechi mbili za NBC Yanga ilipoteza pointi sita mazima na ukuta uliruhusu mabao manne huku safu ya ushambuliaji ikifunga bao moja pekee ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Tabora Unitedbaada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 1-3 Tabora United.
Mashujaa kutoka Kigoma watawakaribisha Kagera Sugar mchezo unaotarajiwa kuchezwa saa 10:00 kwa wababe hao kuwa uwanjani kusaka pointi tatu muhimu.