YANGA YATUMA UJUMBE HUU KWA NAMUNGO

 MCHORA ramani wa Yanga ameweka wazi kuwa wanakabiliwa na mchezo mgumu kesho na watapambana kupata pointi tatu muhimu unatarajiwa kuchezwa saa 12:30 jioni.

Sead Ramovic amebainisha kuwa maandalizi yapo vizuri na wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa na malengo ni kuona wanapata pointi tatu muhimu.

“Tuna mchezo mgumu mbele yetu, katika maandalizi yetu mpaka sasa kila kitu kipo vizuri, tunafahamu Namungo wana wachezaji wazoefu lakini sisi hatupo hapa kutafuta kingine zaidi ya alama tatu.

 “Ni jambo la kujivunia kuwa hapa, nawashukuru mashabiki wa Yanga wanaotoka Dar. Mashabiki wamekuwa na moyo kwa kuwa wapo pamoja na timu kila mahali hivyo nasi tunapaswa kuwapa furaha kwa kupata ushindi.”

Kwa upande wa nyota wa Yanga, Dennis Nkane amesema kuwa wachezaji wanatambua umuhimu wa mchezo huo na wapo tayari kupata pointi tatu.

 

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.