TAMBO zimetawala kwa vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba kwa kubainisha kuwa licha ya kukutana na ushindani mkubwa kwenye mechi za hivi karibuni bado walipambana na kupata ushindi ndani ya uwanja.
Ipo wazi kwamba kikosi cha Simba bado hakijawa kwenye ubora wa asilimia 100 kutokana na wachezaji wake wengi kuwa ni wageni huku Kocha Mkuu Fadlu Davids akibainisha kuwa kuna vitu vidogo vya kufanyia kazi.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa ushindi kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Bravos ni heshima kwa taifa na kuwapa raha mashabiki licha ya kukosa nafasi ambazo walizipata kwenye mchezo huo.
“Unaona namna mchezo ulivyokuwa na ugumu mkubwa mwanzo mwisho, wachezaji walikuwa wanajua wapo vitani hasa ukizingatia kuna timu ilicheza kimataifa ikaleta aibu kubwa kwa taifa hivyo balaa lilikuwa nzito na tukafanikiwa kupata ushindi kwenye mchezo wetu.
“Ambacho kipo ni kuona kwamba tunakuwa kwenye mwendelezo wa ushindi na kuwapa furaha mashabiki wetu wa Simba ambao wapo pamoja nasi bega kwa bega haikuwa rahisi kushinda lakini tumepata ushindi na furaha imebaki kwetu.
“Naskia wanasema ushindi wa penati sio ushindi, nakwambia kwamba sio kazi rahisi ingekuwa rahisi kupata penati basi hata wapinzani wetu wangefunga unaona namna Moussa Camara alivyookoa, yule ni kipa wa mpira kaka.”
Simba Novemba 27 2024 iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bravos mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ikiwa ni hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.