WAKATI familia ya michezo Novemba 27 2024 wakiwa kwenye shangwe la ushindi baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 1-0 Bravos ya Angola kulikuwa na kivumbi kingine cha ushindi kwa wakazi wa kata ya Vingunguti na vitongoji vyake.
Ipo wazi kwamba Novemba 27 2024 kulikuwa na uchaguzi wa Serikali za mitaa hilo pia lilikuwa likihamasishwa pia na Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ambaye aliweka wazi kuwa ratiba asubuhi ni kwenye uchaguz wa Serikali za Mitaa kisha safari Uwanja wa Mkapa kuishangilia Simba.
Wanafamilia ya Michezo Tanzania walitimiza jambo hilo wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan yeye alipanga foleni na Wananchi, Chamwino mkoani Dodoma wakati akielekea kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika nchi nzima.
Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo akiwa yeye alikuwa na wananchi wa Kijiji cha Chema kilichopo Kata ya Bupandwa Halmashauri ya Buchosa katika uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa Novemba 27. Ikumbukwe kwamba Shigongo ni mwanafamilia ya michezo pia aliwahi kuwa na mashindano yaliyokwenda kwa jina la Shigongo Cup.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar ambaye ni Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto yeye naye anni mwanafamilia ya michezo aliwaongoza wana CCM na Wananchi wa mtaa wa Mtambani kupiga kura na mwisho kufurahia ushindi kwa kushinda mitaa 6 na wajumbe wote wa Serikari ya Mtaa waliopo Kata ya Vingunguti.
Kumbulamoto mashindano yake ya hivi karibuni kwenye upande wa michezo yalikuwa yanaitwa Kumbilamoto Cup na alitoa zawadi ya jezi kwa timu zote shiriki pamoja a vifaa vya michezo.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.