SIMBA YASHINDA KWA MKAPA KIMATAIFA, CAMARA KATIKA UBORA

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bravos ya Angola kwenye mchezo wa hatua ya makundi, Kombe la Shirikisho Afrika.

Ni bao la Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba limepachikwa dakika ya 27 kwa mkwaju wa penalti akitumia mguu wake wa kulia akiwa ndani ya 18.

Kipindi cha pili Bravos walikuja kwa kasi kuliandama lango la Simba ambapo walikuwa wakisaka bao na walipata penalti dakika ya 47 iliyosababishwa na Kibe Dennis kwenye harakati za kuokoa mpira ndani ya 18.

Shukrani kwa Mousa Camara kipa namba moja wa Simba ambaye aliokoa penalti hiyo dakika ya 48 na kuliweka lango salama la Simba kwenye kipindi cha pili huku wachezaji wa Simba wakionekana kukosa utulivu kumalizia nafasi wanazopata.

Miongoni mwa nafasi ambazo walizipata ni kupitia kwa Edwin Balua, Mutale ambaye alikuwa ni mchezaji anayepoteza mara kwa mara mipira kwa kucheza faulo ama kuchezewa faulo.

Hili ni bao la kwanza na Ahoua kwenye anga la kimataifa akiwa na uzi wa Simba kwenye hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.