HII HAPA KAZI YA WANASIMBA, KIMATAIFA KWA MKAPA

AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanachama wa Simba leo ni sikukuu yao kwa kufanya mambo makubwa mawili, mapema kupiga kura kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa kisha jambo la pili kukutana Uwanja wa Mkapa kuishangilia Simba saa 10:00 jioni.

Simba ina inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids inakibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Bravos mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ambapo wababe wote wawili kwenye hatua ya makundi kimataifa wanasaka pointi tatu.

Ally amesema ushindi wa Simba ni ushindi wa taifa zima hivyo il kuwapa nguvu wachezaji kupambania pointi tatu lazima wajitokeze kwa wingi kushangilia vibayavibaya.

“Kuna kazi kubwa yakufanya Novemba 27 ambayo itakuwa ni siku ya mapumziko kinachotakiwa kufanyika asubuhi mashabiki na wanachama wa Simba wanapaswa kupiga kura kuchagua viongozi wa Serikali za Mtaa baada ya hapo safari inakuwa kwenda Uwanja wa Mkapa.

“Uwanja wa Mkapa kazi inakuwa moja kuishangilia Simba ipate matokeo kwa kuwa ushindi wa Simba ni furaha kwa kila mmoja na muda ni sasa kufanya hayo inawezekana na wachezaji wanapenda kuwapa furaha mashabiki. Tujitokeze kwa wingi Uwanja wa Mkapa.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.