PATRICK Aussems maarufu kama Uchebe hatakuwa ndani ya kikosi cha Singida Black Stars pamoja na Dennis Kitambi aliyekuwa msaidizi wake baada ya kukutana na Thank You Novemba 25 2024.
Kwa sasa timu hiyo itakuwa chini ya Mkurugenzi wa Ufundi, Ramadhani Nswanzurwimo lama kocha mkiu wakati akitafutwa kocha mwingine. Mechi 11 nafasi ya nne, pointi 24 ushindi mechi 7, sare 3 poteza mchezo mmoja.
Hizi hapa mechi zake tatu zilizotajwa kuwa sababu kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa timu hiyo umebainisha kuwa mwenendo wa mechi tatu za mwisho haukuwa bora kwa benchi la ufundi.
Katika msako wa pointi tisa ni mbili ilivuna kwa sare mbili na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Yanga ikiwa nyumbani msimu wa 2024/25.
Oktoba 30 2024 ilikuwa ni Singida Black Stars 0-1 Yanga ulichezwa Uwanja wa New Amaan Complex ambapo hapo walipoteza pointi tatu mazima wakiwa nyumbani kwa bao la Pacome.
Novemba 2 2024 ubao wa Uwanja wa New Amaan Complex ulisoma Coastal Union 0-0 Singida Black Stars walikuwa ugenini wakigawana pointi mojamoja katika mchezo wa ligi.
Novemba 25 2024, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora United 2-2 Singida Black Stars ikumbukwe kwamba katika mchezo huu dakika 45 za awali Singida Black Stars walikuwa wanaongoza 2-1.
Mabao yalifungwa na Elvis Rupia dakika ya 15 na mwamba wa kumwita Trabi mwisho ikawa 2-2 wakigawana pointi mojamoja ugenini.
Ikumbukwe kwamba ndani ya Oktoba nyota aliyekuwa akitundishwa na Uchebe, Marouf Tchakei alichaguliwa kuwa mchezaji bora ambapo katika mechi nne alikomba dakika 360, mabao matatu na pasi moja.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.