YANGA YAWAITA MASHABIKI KIMATAIFA

NAHODHA wa Yanga, Bakari Nondo amesema kuwa matokeo yaliyopita kwenye mechi za ligi hayajawaondoa kwenye reli hivyo watapambana kupata matokeo kwenye mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Yanga kwenye mechi mbili za ligi mfululizo ambazo ni dakika 180 ilipoteza ilikuwa Yanga 0-1 Azam FC kisha kete ya pili ilikuwa Yanga 1-3 Tabor United kwenye msako wa pointi sita ilipishana nazo mazima na mpanga mipango Miguel Gamondi alikutana na Thank You.

Kesho, Novemba 26 Yanga ambayo kwa sasa ipo chini ya Kocha Mkuu, Sead Ramovic raia wa Ujerumani ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa makundi Ligi ya Mabingwa Afrika ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa kocha mpya ndani ya Jangwani.

Nondo amesema: “Matokeo ya mechi zilizopita ni mechi za Ligi hivyo makosa tumefanyia kazi na sasa hivi tunakwenda kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Niwaombe mashabiki waondoe hofu na waje kwa wingi uwanjani. Tusahau yaliyopita na kesho tuanze safari nyingine.

“Kwa muda mchache tuliokaa na mwalimu yako mambo ametupa na tumeyaelewa sisi wachezaji kiujumla kesho naamini mtakuja kuona mpira tofauti na ladha ya tofauti kutoka kwetu mashabiki hakika tutawapa furaha..

“Tunaelewa mechi itakuwa ngumu, lakini sisi tumejiandaa vizuri na ninaamini tutakwenda kupambana kwa ajili ya timu yetu na mashabiki wetu. Niwaombe mashabiki waje kwa wingi na kutushangilia kwa dakika zote 90 tutakazokuwa tunapambana uwanjani.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.