UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa unatambua ugumu uliopo kwenye mchezo wao dhidi ya Bravos ya Angola ila mpango mkubwa ni kupata pointi tatu Uwanja wa Mkapa.
Ni Novemba 27 2024 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa ikiwa ni hatua ya makundi. Simba ipo chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids aliyetoka kuvuna pointi tatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Pamba Jiji.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa mashabiki ni muda wao kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa kuwapa nguvu wachezaji kusaka ushindi kwenye mchezo huo ambao utakuwa ni mgumu.
“Tumekuwa na mwendelezo wa matukio kwenye wiki hili unaona tuliwashika mkono Watoto Yatima Mbweni kwenye kituo cha Mwandaliwa ikiwa ni mwendelezo wa kurejesha kwa jamii tukishirikiana na Modewji Foundation.
“Leo mwendelezo wa hamasa tumetoa damu ikiwa ni sadaka kwa Mungu kwani hii itawasaidizi Watanzania wengi, lakini kikubwa ni Jumatano kwenye mchezo wetu dhidi ya Bravos ambacho tunahitaji ni kupata ushindi.
“Mashabiki ni muda wa kujitokeza kwa wingi kuwapa nguvu wachezaji kusaka ushindi kwani uwepo wenu ni muhimu na tunahitaji kupata pointi tatu tukiwa Uwanja wa Mkapa inawezekana.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.