KWENYE eneo la makipa ndani ya kikosi cha Simba, kipa namba moja Mousa Camara amejenga utawala wake akiwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Wakati Simba ikicheza mchezo wa 11 dhidi ya Pamba Jiji, Novemba 22 2024 Uwanja wa Kirumba, Mwanza alianza kikosi cha kwanza.
Unakuwa ni mchezo wa 11 wa NBC Premier League kwa Camara kuanza kikosi cha kwanza na benchi alikuwa yupo mwamba Ally Salim ambaye hajapata nafasi ya kucheza msimu wa 2024/25.
Kumekuwa na ushindani mkubwa wa namba hasa eneo la mlinda mlango ambapo kwa Yanga na Simba wenye uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza ni makipa wageni.
Camara ni namba moja kwa makipa ambao hawajafungwa mechi nyingi akiwa hajafungwa kwenye mechi 9 huku mechi mbili akiruhusu kufungwa.
Dhidi ya Pamba Jiji aliokoa hatari tatu za moto zilizokuwa zinakwenda kwenye lango lake na mwisho ubao ulisoma Pamba Jiji 0-1 Simba kwa bao la Leonel Ateba dakika ya 22 kwa mkwaju wa penalti.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.