Ligi Kuu ya Tanzania Bara inaendelea tena leo Jumamosi, Novemba 23, 2024, ambapo Matajiri wa Chamazi, Azam FC, watakuwa nyumbani kuwakaribisha Wanankurukumbi, Kagera Sugar, katika Uwanja wao wa Chamazi Complex.
Mchezo wa Azam FC dhidi ya Kagera Sugar utapigwa saa 1:00 usiku.
Michezo mingine ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayopigwa leo:
• Saa 8:00 mchana, KenGold watakuwa nyumbani Uwanja wa Sokoine, Mbeya, wakiwakaribisha Wagosi wa Kaya, Coastal Union.
• Saa 10:15 jioni, Wanamapigo na Mwendo, Mashujaa FC, watakuwa Uwanja wa Lake Tanganyika wakiwaalika Namungo FC.