SEHEMU ya uongozi wa Yanga SC, ikiongozwa na Rais wa klabu hiyo Hersi Said, umefika jijini Dodoma ukiwa safarini kwenda Kibaigwa.
Yanga ikishirikiana na Mdhamini na Mfadhili wa timu hiyo Ghalib Said Mohamed, wanakwenda Kibaigwa kutoa msaada kwa wenye uhitaji ikiwa ni sehemu ya hamasa kuelekea mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal ya Sudan.
Mechi hiyo itapigwa Novemba 26, saa 10:00 jioni
Official Website