SIMBA, YANGA CHALI MCHUJO WA KLABU BORA YA MWAKA

Shirikisho la soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya vilabu vitano vinavyowania tuzo ya klabu bora ya mwaka huku vigogo wa Tanzania Simba Sc na Yanga Sc wakipitiwa na panga la CAF baada ya mchujo.

Baada ya mchujo wa vilabu 10, sasa vimebakia vilabu vitano ambazo ni AL Ahly, Zamalek Fc ya Misri, RS Berkane ya Morocco, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Esperance De Tunis ya Tunisia.

Vilabu vilivyoondolewa kwenye kinyang’anyiro hicho Simba , Young Africans , Dreams Fc , Petro Atletico na Tp Mazembe .