KUFUZU AFCON 2025: STARS KUCHEZA DHIDI YA GUINEA KWENYE UWANJA WA MKAPA

Leo, Stars itacheza mchezo wa mwisho wa kufuzu Afcon 2025 dhidi ya Guinea kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa utakaoanza saa 10:00 jioni.

Ni mchezo wa lazima Stars kushinda ili kufuzu michuano hiyo itakayofanyika mwakani nchini Morocco huku tumaini la Watanzania wengi ni uwepo wa nahodha, Mbwana Samatta na Simon Msuva.