FOUNTAIN GATE INAVUTIA NA KUSHANGAZA

NDANI ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2024/25 ushindani ni mkubwa ambapo kila timu inapambana kufanya kweli ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani.

Vinara wa ligi ni Simba chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids imekuwa na mwendo wake ambapo kwenye mechi 10 imepoteza mchezo mmoja dhidi ya Yanga.

Kuna Fountain Gate hii imekuwa na rekodi nzuri na zile ambazo zinashangaza kutokana na kuwa timu namba mbili kufunga mabao mengi na inaingia kwenye orodha ya timu iliyofungwa mabao mengi pia.

Fountain Gate kwenye msimamo ni nafasi ya tano jambo ambalo sio dogo huku ikiwa imefunga jumla ya mabao 20 ikiwa ni namba mbili kwa timu zenye mabao mengi.

Ikumbukwe kwamba vinara ni Simba kwenye upande wa kufunga mabao mengi ikiwa na mabao 21 baada ya kucheza mechi 10.

Kinara wa utupiaji kwenye ligi anatoka Fountain Gate  anaitwa Suleiman Mwalimu akiwa ametupia mabao sita namba mbili ni Jean Ahoua huyu ametupia mabao matano.

Fountain Gate ipo juu ya Yanga iliyotupia mabao 14 tofauti ya mabao sita na imewaacha Azam FC wenye mabao 13 kama ilivyo Singida Black Stars tofauti ya mabao 7.

Ajabu imefungwa mabao 20 baada ya kucheza mechi 11 ndani ya ligi kwa msimu wa 2024/25 hivyo ina kazi kubwa kuongeza nguvu eneo la ulinzi ambalo limeonekana kutokuwa imara.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.