MECHI 10 Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids imecheza huku ikambulia joto ya jiwe kwa kufungwa mchezo mmoja dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilikuwa Kariakoo Dabi na sare ni mchezo mmoja.
Hizi hapa rekodi za mechi 10 za Simba ndani ya 2024/25 kwenye NBC Premier League namna hii:-
Simba 3-0 Tabora United mchezo huu ulichezwa Uwanja wa KMC, Mwenge ilikuwa Agosti 18 2024 ni mchezo wa kwanza kwa Simba kwenye ligi na mtupiaji bao la kwanza ni Che Malone ilikuwa dakika ya 14.
Simba 4-0 Fountain Gate, huu ulikuwa ni mchezo wa pili kwa Simba ulichezwa Uwanja wa KMC, Mwenge ilikuwa Agosti 25 2024.
Azam FC 0-2 Simba huu ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Simba kucheza ugenini ulichezwa Uwanja wa New Amaan Complex Septemba 26 2024.
Dodoma Jiji 0-1 Simba ilikuwa Septemba 29 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma walisepa na pointi tatu kwenye mchezo huu.
Simba 2-2 Coastal Union kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC, Mwenge ilikuwa ni Oktoba 4 2024.
Simba 0-1 Yanga ni Oktoba 19 2024 kwenye Kariakoo Dabi, Simba ilipoteza pointi tatu kwa bao la kujifunga lake Kelvin Kijili, Uwanja wa Mkapa.
Tanzania Prisons 0-1 Simba ilikuwa Uwanja wa Sokoine, ilikuwa ni Oktoba 22 2024.
Simba 3-0 Namungo ilikuwa Uwanja wa KMC, Mwenge, Oktoba 25 2024.
Mashujaa 0-1 Simba, Novemba Mosi 2024, Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Simba 4-0 KMC ilikuwa Novemba 6 2024 Uwanja wa KMC, Mwenge.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.