MABINGWA WATETEZI WAMTAMBULISHA BOSI MPYA

ABDULHAMID Moalin ametambulishwa kuwa bosi mpya ndani ya kikosi cha Yanga kwene eneo la masuala ya ufundi kwa msimu wa 2024/25.

Moalin alikuwa Kocha Mkuu wa KMC inayotumia Uwanja wa KMC Complex na mchezo wake wa mwisho kukaa benchi ilikuwa dhidi ya Simba uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.

Baada ya dakika 90 uba ulisoma Simba 4-0 KMC alifikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake wa mwaka mmoja na mabosi hao kisha akawa anatajwa kuwa atakuwa kocha msaidizi ndani ya kikosi cha Yanga.

Taarifa rasmi ambayo imetolewa na Yanga kupitia ukurasa wa Instagram umemtambulisha kocha huyo kuwa atakuwa Mkurugenzi wa Ufundi ndani ya kikosi cha Yanga.

Ikumbukwe kwamba Sead Ramovic huyu ametambulishwa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga akichukua mikoba ya Miguel Gamondi ambaye amekutana na Thank You, msimu wa 2023/25 Gamondi alikiongoza kikosi cha Yanga kutwaa ubingwa hivyo ni mabingwa watetezi.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.