WAZIRI MKUU MAJALIWA AFIKA LILIPOPOROMOKA JENGO KARIAKOO – ATOA TAMKO la SERIKALI…

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kushirikiana na Kamati za Ulinzi kuhakikisha manusura waliofukiwa na kifusi cha ghorofa lililoporomoka Wanaokolewa

Aidha, Waziri Mkuu ameagiza Mitungi ya Hewa ya #Oxygen ipelekwe kwenye eneo hilo ili kuwasaidia manusura waliopo chini ambao bado hawajaokolewa wakati zoezi la uokozi likiendelea

Hadi sasa watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia huku wengine (idadi haijajulikana) wakiwa bado wamefukiwa chini baada ya jengo lenye ghorofa 4 kuanguka leo Novemba 16, 2024 ambapo Vikosi vya Jeshi la Wananchi na Zimamoto vikiendelea na uokoaji.