SIMBA KWENYE REKODI YAKIMBIZA BONGO

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi kimepeta kwenye rekodi ndani ya 2024/25 kutokana na kufanya vizuri kwa wachezaji baada ya mechi 10.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa hayo yote yanatokana na uwekezaji ambao umefanywa kwa kuchukua wachezaji wenye ubora mkubwa.

“Tuna wachezaji wenye namba nzuri huu ni mpira na kila mmoja anapenda kuona rekodi kwa wachezaji wetu kila kona yaani hapa Simba mpaka beki anafunga unamjua Mohamed Hussen beki wa mpira? Huyu amefunga bao lake safi kwenye ligi.

“Kuna Jean Ahoua yeye kafikisha mabao matano na pasi nne za mabao, Awesu Awesu kafunga mabao mawili kwenye ligi sasa kila mchezaji unayemuona Simba anatembeza ubaya ubwela halafu kuna kipa Mussa Camara anadaka vibaya mno.”

Camara kwenye mechi 10 ambazo amecheza hajafungwa kwenye mechi 8 akiwa ni namba moja kwa makipa ambao hawajafungwa mabao mengi.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.