Klabu ya KMC FC, imemtangaza Kali Ongala kuwa Mkuu mpya wa timu hiyo, baada ya kuondoka kwa aliyekuwa kocha Mkuu, Abdihamid Moalin.
Akiwa kama kocha, Kali amewahi kuifundisha klabu ya Azam FC, lakini pia akiwa kama mchezaji amewahi kuzichezea klabu kama Azam FC, Yanga SC, GIF Sundsvall na nyingine kadhaa.
“Uamuzi wa kumchagua Kali Ongala umefikiwa baada ya Bodi ya klabu kufanya kikao na kupitia CV za makocha mbalimbali na kumpitisha Ndugu Kali Ongala” ilisema taarifa ya KMC FC.