ISHU YA GAMONDI NA THANK YOU UPEPO UPO HIVI

WAKATI kukiwa na fukuto kwamba huenda Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga atakutana na mkono wa Thank You, kocha huyo bado yupoyupo kwa kuwa ameanza kuwanoa wachezaji wa timu hiyo kuelekea mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga imetinga hatua ya makundi ambapo inatarajiwa kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga hilo na itakuwa na kazi dhidi ya Al Hilal ya Sudan mchezo unaotarajiwa kuchezwa Novemba 26 2024.

Tetesi zinaeleza kuwa Gamondi yupo kwenye hesabu za kusitishiwa mkataba wake wa mwaka mmoja aliongeza kutokana na mwendo wa timu hiyo kutokuwa bora ndani ya msimu wa 2024/25 ambapo timu hiyo imepoteza mechi mbili mfululizo.

Wakati tetesi zikieleza hivyo tayari Yanga imerejea mazoezini kwa maandalizi ya mechi za kimataifa ambapo ni Gamondi anawapa mbinu wachezaji wake hivyo inamaanisha kwamba bado yupoyupo ndani ya Yanga.

Kocha huyo amekuwa akitajwa kuwa hana maelewano mazuri na baadhi ya wachezaji ndani ya kikosi hicho jambo ambalo limekuwa likiweka matabaka ndani ya timu hiyo jambo ambalo linatajwa kuwa sababu ya kibarua chake kuwa kwenye kuti kavu.

Hata hivyo Yanga hawajatoa taarifa yoyote kuhusu kocha Gamondi zaidi ya kutoa taarifa kuwa wamehama Uwanja wa Azam Complex na sasa watatumia Uwanja wa KMC Complex.

Taarifa kutoka Yanga zimeeleza kuwa Gamondi bado yupo ndani ya kikosi hicho ndio maana anawafundisha wachezaji kuelekea mechi za kitaifa na kimataifa.

“Masta Gamondi bado yupo ndani ya Yanga hivyo hayo ni maneno ya kututoa kwenye reli tupo imara na kocha tupo naye.” ilieleza taarifa hiyo.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.