Mashabiki wakubashiri wa kampuni inayotamba ya LEONBET Tanzania walipata
burudani ya kisasa ya kuvunja mbavu na wachekeshaji maarufu nchini kwenye uzinduzi rasmi
wa kampuni hiyo uliopewa jina la CHEKA TU: LEONBET EDITION.
Burudani hiyo ya kisasa ilifanyika Novemba 8, 2024 kwenye ukumbi wa Warehouse Masaki. Mashabiki wa vichekesho nchini walipata burudani kutoka kwa wakali wa Cheka Tu, akiwemo Coy
Mzungu, Ndaro, Asma, Mtumishi Obama, na Chard Talent, ambao walihakikisha kuwa kila aliyehudhuria
anatabasamu na kufurahia uzinduzi huo.
Burudani zaidi zilifuatia kwa muziki wa moja kwa moja kutoka kwa wasanii wakubwa wa Tanzania,
akiwemo Maua Sama na Jaivah, ambao walifanya tamasha kuwa la kukumbukwa kwa mashabiki wote.
Katika tukio hilo, Meneja Mkuu wa LEONBET Tumaini Maligana pamoja Mkurugenzi wa Operesheni wa Kanda ya Afrika kwa LEONBET, Jérôme J. Dufourg walikuwepo katika burudani hiyo. Viongozi hao wakuu wa LEONBET Tanzania waliwashukuru mashabiki wote waliofika katika uzinduzi huo na kuwapa sapoti kubwa.
Maligana, alitoa shukrani za dhati kwa wote waliojitokeza na kwa kuunga mkono uzinduzi wa
brand yao.
“Ningependa kuchukua muda mfupi tu kuitambulisha brand yetu ya LEONBET – Simba La Mikeka.
LEONBET ni kampuni ya michezo ya ubashiri iliyoingia rasmi Tanzania ili kuambatanisha burudani
ya kubashiri kwenye michezo na slots na kutoa fursa ya kutengeneza pesa,” alisema,
Kwa upande wake, Dufourg, akiwakilisha mtazamo wa kimataifa wa LEONBET, alisisitiza dhamira ya
kampuni hiyo ya kuleta uzoefu bora wa michezo ya kubashiri kwa Tanzania.
“Tunafuraha sana kuja Tanzania, tukijua kuwa tuna historia na uzoefu wa miaka 15 katika sekta hii, na
tunayo dhamira ya kutoa huduma ya kiwango cha juu kwa wateja wetu. Tunaleta si tu ubashiri bali
burudani ya hali ya juu kwa wateja wetu nchini Tanzania,” alisema Dufourg.
Dufourg aliendelea kueleza jinsi LEONBET inavyoweka msisitizo mkubwa kwenye huduma bora
za wateja ambapo alisema:- “Tunataka kuhakikisha kwamba mteja anafurahia uzoefu wake bila tatizo lolote. Kutoka kwa malipo ya haraka, tovuti yenye kasi, hadi bonasi nyingi, tuko
hapa ili kurahisisha na kuboresha kila sehemu ya uzoefu wa kubeti na kucheza kasino,” aliongeza.
Maligana na Dufourg walifurahia kuwakilisha LEONBET kama sehemu ya mtindo wa maisha kwa
wapenzi wa michezo na burudani.
Maligana, alieleza kuwa, kwa kujiunga na LEONBET, wateja wanaweza kufurahia ofa
mbalimbali mara tu wanapojisajili. “Tuna ofa kibao kwa ajili yako ukijiunga na LEONBET. Ukijisajili tu, unapokea ofa ya kipekee!” alisema.
Alisema kuwa uzinduzi wa LEONBET umeacha alama kubwa kwa mashabiki wa vichekesho na
wapenzi wa michezo ya kubashiri nchini Tanzania, na kuthibitisha kuwa LEONBET ni zaidi ya
kubeti—ni sehemu ya burudani na maisha kwa watanzania wote.