SIMBA ISHU YA PACOME IPO NAMNA HII

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa ikiwa wataridhishwa na kiwango cha nyota wa Yanga, Pacome Zouzoua utahangaika naye ili kupata saini yake.

Nyota huyo mkataba wake unatarajiwa kugota mwisho mwishoni mwa msimu wa 2024/25 ambapo bado hajaongeza kandarasi nyingine  huku mazungumzo yakitajwa kuendelea.

Ahmed Ally Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema wanatambua mkataba wa Pacome unaisha na hajaongeza bado hivyo wanaangalia kiwango chake.

“Ikiwa Pacome kiwango chake kitakuwa katika ubora basi tutahangaika naye kwani tunajua bado hajaongeza mkataba mwingine. Tunatambua kwamba ni mchezaji mzuri hivyo tukiona kiwango chake ni bora basi itakuwa hivyo.”

Simba baada ya kucheza mechi 10 ni pointi 25 imekusanya nafasi ya kwanza kwenye msimamo inafuatiwa na Yanga nafasi ya pili ikiwa na pointi 24.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.