RACHID Taoussi, Kocha Mkuu wa Azam FC amechaguliwa kuwa kocha bora ndani ya Oktoba baada ya kuingia fainali na kuwashinda makocha wengine ambao alikuwa akipambanishwa nao.
Taarifa imeeleza kuwa kocha huyo aliyekiongoza kikosi hicho kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga amewashinda Abdulhamid Moalin wa KMC na Denis Kitambi wa Singida Black Stars.
Rekodi zinaonyesha kuwa Taoussi aliongoza timu ya Azam FC kuvuna ushindi kwenye mechi tatu ambazo ni dakika 270 ilikuwa Namungo 0-1 Azam FC, Tanzania Prisons 0-2 Azam FC na Azam FC 4-1 Ken Gold.
Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imeeleza kuwa kocha huyo aliipandisha Azam FC nafasi moja kutoka ya tano mpaka ya nne kwa msimu wa 2024/25.
Mbali na kocha huyo kusepa na tuzo hiyo ile ya mchezaji bora ndani ya Oktoba ipo kwa nyota Marouf Tchakei wa Singida Black Stars akiwashinda Pacome wa Yanga na Lusajo Mwaikenda wa Azam FC.
Nyota huyo alihusika kwenye mabao manne ndani ya dakika 360 akifunga mabao matatu kwenye mechi ambazo alicheza na kutoa pasi moja ya bao. Mechi hizo ilikuwa Mashujaa 0-1 Singida Black Stars, Singida Black Stars 2-0 Namungo, Singida Black Stars 2-0 Fountain Gate na Singida Black Stars 0-1 Yanga.
Singida Black Stars ilifunga mabao matano kwenye mechi nne huku nyota huyo akifunga mabao matatu ndani ya uwanja kwenye mechi hizo.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.