AWESU AWESU ATUMA UJUMBE HUU KWA MABOSI KMC

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Awesu Awesu amebainisha kuwa mzunguko wa pili ikiwa atawafunga mabosi wake wa zamani KMC atashangilia bao hilo kwa kuwa bao la kwanza hakushangilia.

Nyota huyo kwenye mchezo wa kwanza kukutana na mabosi zake KMC kwenye ligi ilikuwa ni Novemba 6 2024 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 4-0 KMC ambapo bao la ufunguzi alifunga yeye dakika ya 25 akitumia pasi ya Steven Mukwala, baada ya kufunga hakushangilia.

Awesu amesema kuwa hakushangilia bao hilo kutokana na heshima aliyopewa na timu yake hiyo ya zamani KMC jambo lililotoa nafasi kwake yeye kusajiliwa na Simba ambayo anaichezea kwa wakati huu.

“Nilipata thamani kubwa kutoka timu yangu ya KMC jambo hilo lilinifanya nishangilie nilipowafunga na kuwaomba msamaha kwa kuwa hii ni kazi. Lakini ikitokea kwenye mechi nyingine nikafunga basi nitashangilia.

“Mchezo wetu dhidi yao tulitarajia kwamba utakuwa mgumu na ilikuwa hivyo, unajua mechi zote za Simba sio nyepesi kikubwa ni maandalizi mazuri na kupata pointi tatu muhimu.”

Simba kwenye msimamo ni namba moja baada ya kucheza mechi 10 imekusanya pointi 25 inafuatiwa na Yanga yenye pointi 24 kibindoni.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.