MUUAJI wa Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Offen Chikola amesema kuwa furaha kubwa kupata pointi tatu mbele ya timu kubwa kutokana na mchezo wao kuwa mgumu mwanzo mwisho ndani ya uwanja.
Yanga chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi imepoteza mchezo wa pili ikiwa nyumbani msimu wa 2024/25 ambazo ni dakika 180.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex umesoma Yanga 1-3 Tabora United, mabao ya Offen Chikola dakika ya 19 na 45 huku lile la tatu ni Nelson Muganda katupia dakika ya 77 ilikuwa ni Novemba 7 2024.
Clement Mzize amepachika bao pekee la Yanga dakika ya 90. Ikumbukwe kwamba Novemba 2 2024 ilikuwa Yanga 0-1 Yanga, Novemba 7 2024, Yanga 1-3 Tabora United. Mchezo wa kwanza Yanga imepoteza ikiwa nyumbani na mchezo wa pili pia ikiwa nyumbani.
Chikola ameweka wazi kuwa walikuwa wanatambua aina ya timu ambayo wanakwenda kukutana nayo jambo ambalo walifanyia kazi eneo la mazoezi na kuwa tayari kutafuta ushindi.
“Tulitambua tunakwenda kukutana na timu ya aina gani lakini mwisho wa siku imekuwa siku nzuri kwetu na kupata matokeo mazuri ambayo ni pointi tatu hizi ni zawadi kwa mashabiki wa Tabora United na wale ambao wanapenda mpira mzuri.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.