YANGA WANATAMBUA WANAKUTANA NA TIMU YA NAMNA GANI

WACHEZAJI wa Yanga wamebainisha kwamba wanatambua wanakutana na timu ya namna gani uwanjani hivyo watapambana kufanya vizuri ili kupata matokeo mazuri ndani ya uwanja kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Yanga ni namba mbili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 9 huku safu ya ulinzi ikiwa imeruhusu bao moja pekee ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex Novemba 2 2024.

Nickson Kibabage beki wa kupanda na kushuka kwa niaba ya wachezaji wa Yanga amebainisha kwamba wanatambua aina ya timu ambayo wanakwenda kukutana nayo jambo ambalo limewafanya wajipange kwa umakini.

Nyota huyo amesema mchezo uliopita makosa benchi la ufundi lilifanyia kazi na wamesahau matokeo yaliyopita hesabu kubwa ni kupata matokeo mazuri kwenye mchezo ujao.

“Kwa upande wetu safu ya ulinzi tunafahamu tunakwenda kukutana na safu ya ushambuliaji ya aina gani, kuna wachezaji wazuri kama Herithier Makambo, Yacouba Sogne hilo linajulikana na mwalimu wetu anajua pia na ameshafanya tathmini namna gani yakucheza dhidi yao.

“Kazi yetu sisi kama walinzi ni kufuata maelekezo ya mwalimu tunajua kwamba wapinzani wetu watafanya mara mbili zaidi kupata alama hivyo lazima tujiandae vema.”

Ni pointi 14 wamekusanya Tabora United baada ya kucheza mechi 10 wanakutana na Yanga wenye pointi 24 baada ya kucheza mechi 9 msimu wa 2024/25.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.