KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amebainisha kuwa wanahitaji pointi tatu dhidi ya Tabora United kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex Novemba 7 2024 kupata nafasi ya kuongoza ligi ambayo ina ushindani mkubwa huku vinara wakiwa ni Simba.
Yanga ambao ni mabingwa watetezi baada ya kucheza mechi 9 imepoteza mchezo mmoja ilikuwa Novemba 2 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 0-1 Azam FC bao la ushindi kwa Azam FC lilifungwa na Gibril Sillah dakika ya 33.
Masta Gamondi amebainisha kuwa wana kazi kubwa ya kufanya kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Tabora jambo ambalo wamelifanyia kazi kwa umakini mkubwa hivyo wataingia uwanjani kwa tahadhari kusaka ushindi mbele ya wapinzani wao hao.
“Tuna mchezo mgumu dhidi ya Tabora United, tumewafuatilia wapinzani wetu sio timu mbaya ni nzuri hasa kwenye mechi zake zilizopita ilipata matokeo hii ina maana kwamba wamekuwa kwenye ubora kwa hivi karibuni tunalitambua hilo.
“Ushindi kwenye mchezo wetu utatupa nafasi ya kuwa namba moja kwenye ligi hii inamaanisha kwamba ili tuongoze ni lazima tushinde. Tumefanya maandalizi mazuri na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu.”
Yanga imekusanya pointi 24 baada ya mechi 9 kwenye msimamo ni nafasi ya pili huku kinara akiwa ni Simba mwenye pointi 25 baada ya kucheza jumla ya mechi 10 kwenye ligi.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.