AZAM FC WATAMBA KUENDELEA NA KASI

UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa utaendelea na kasi yao kwenye mechi zijazo za ushindani ndani ya msimu wa 2024/25 kutokana na ubora walionao.

Ipo wazi kwamba Azam FC ni timu ya kwanza kukomba pointi tatu mazima dhidi ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi walipokutana mzunguko wa kwanza Uwanja wa Azam Complex Novemba 2 2024 ubao uliposoma Yanga 0-1 Azam FC.

Bao la ushindi kwenye mchezo huo lilifungwa na Gibrill Sillah dakika ya 33 ambapo alifunga akitumia pasi ya Mtasigwa aliyechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa wanatambua kuna ushindani mkubwa kwenye ligi hilo lipo wazi watafanya kazi kubwa kwenye maandalizi ili kuwa bora kwa mechi zinazofuata kuendelea kwenye kasi yao.

“Kuna mechi nyingi ambazo zipo na tunaamini kwamba ushindani ni mkubwa baada ya Yanga kupata wanachostahili ni muda wa kuendeleza kasi yetu kwenye mechi zinazofuata hilo linawezekana na benchi la ufundi linafanyia kazi makosa yaliyopita kuwa bora zaidi.”

Azam FC kwenye msimamo wa ligi ni nafasi ya 4 ikiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi 10 vinara ni Simba wenye pointi 25 baada ya kucheza mechi 10.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.