AHOUA BADO ANAJITAFUTA HUKO UNYAMANI

LICHA ya kuwa namba moja kwenye wakali wa kucheka na nyavu ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo mdhamini wake mkuu ni NBC huku kwa upande wa matangazo ikiwa ni Azam TV, kiungo Jean Ahoua bado anajitafuta kwa kuwa hajawa katika ubora wake.

Nyota huyo ni namba pekee zinambeba lakini kwenye utendaji hasa timu inapokuwa haina mpira amekuwa hana faida kubwa hivyo anapaswa kuongeza zaidi juhudi ili kuwa imara kwenye mechi zijazo.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo mgumu uliokuwa na matumizi makubwa dhidi ya Yanga alipata maumivu  yaliyomuweka nje kwa muda akipambania hali yake na katika mchezo wa waliotoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 dhidi ya Coastal Union hakuwa kwenye kiwango bora.

Licha ya kufunga mabao mawili Novemba 6 2024 dhidi ya KMC bado Ahoua hakuwa kwenye ubora wake kwa kuwa sio mchezaji anayetisha bali mchezaji mwenye zali la kucheka na nyavu na kutoa pasi ambazo zimekuwa zikileta matokeo kwa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Hivi karibuni Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alisema kuwa bado Ahoua hajafikia kiwango cha asilimia 100 hivyo ana kazi ya kuendelea kucheza kwa umakini kuwa bora zaidi ndani ya uwanja katika kutimiza majukumu yake.

“Bado unaona Ahoua hajafikia asilimia 100 ya ubora wake ni kiasi kidogo amekionyesha hivyo akifikia kwenye ubora wake tutashuhudia mengi Wanasimba hasa kwenye upande wa burudani.”

Novemba 6 2024 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa KMC, Mwenge ulisoma Simba 4-0 KMC huku Ahoua akitupia mabao mawili, Awesu Awesu alifunga bao la ufunguzi na Edwin Balua alitupia bao moja.

Ahoua ni namba moja kwa wakali wa kucheka na nyavu akiwa ametupia mabao matano na pasi nne akihusika kwenye mabao 9 kati ya 21 yaliyofungwa na Simba yenye pointi 25 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.