MSHAMBULIAJI MUKWALA KAZINI TENA

BAADA ya kumaliza kazi kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara, Novemba Mosi 2024 mbele ya Mashujaa ya Kigoma mwisho wa reli, mshambuliaji Steven Mukwala, Leonel Ateba, Awesu Awesu ambaye ni kiungo mshambuliaji leo wana kibarua kingine mbele ya KMC.

Ipo wazi kwamba mchezo uliopita baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Lake Tanganyika ulisoma Mashujaa 0-1 Simba.

Bao la ushindi kwa Simba lilifungwa dakika ya 90 kwa pigo la kichwa akiwa ndani ya 18 akitumia pasi ya Awesu Awesu ambaye alipiga kona katika dakika za lala salama kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani wa mwanzo mwisho.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua mchezo wao dhidi ya KMC ni mgumu watapambana kupata matokeo mazuri ndani ya uwanja.

“Kuna ushindani mkubwa ndani ya uwanja tunatambua kwamba mchezo utakuwa mkubwa na ambacho tunakifanya kwa sasa ni kuwa tayari na kuwaambia Wanasimba wajitokeze kwa wingi kupata burudani kwenye mchezo wetu muhimu.

“Wachezaji wote wapo tayari ni muda wa kazi kubwa kusaka pointi tatu uwanjani, inawezekana kwa kuwa makosa kwenye mechi iliyopita yamefanyiwa kazi na sasa tunakwenda kwenye mchezo wetu muhimu tena kwenye ligi.”

 

 

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.