SIMBA KUKIPIGA JUMATANO LIGI KUU BARA

BAADA ya kupata ushindi kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mashujaa FC katika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma kituo kinachofuata kwa Simba ni Jumatano dhidi ya KMC.

Katika mchezo huo Simba ilipata bao la jioni kupitia kwa mshambuliaji Steven Mukwala ambaye alitumia pasi ya Awesu Awesu katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa na bao lilifungwa dakika ya 90.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa ushindi huo ilikuwa ulikuwa ni muhimu kwao kutokana na uhitaji wa pointi tatu na pongezi kwa wachezaji kwa kufanya kazi kubwa.

“Ulikuwa ni mchezo muhimu na kikubwa ambacho tulikuwa tunahitaji ni pointi tatu jambo ambalo lilifanikiwa hivyo tunawapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa kupambania kuona furaha inakuwa kwa Wanasimba.

Kuhusu mchezo wao ujao dhidi ya KMC, Ally amesema: “Mchezo wetu dhidi ya KMC utapigwa Jumatano saa 10:00 jioni. Wana Simba tujiandae kwa mchezo huu na tuje kwa wingi uwanjani. Burudani zilipo ndani ya timu yetu hivi saaa hupaswi kukosa mechi zetu.”

Simba kwenye msimamo wa ligi ni nafasi ya tatu ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza mechi 9 kinara ni Yanga mwenye pointi 24 baada ya kucheza mechi 9 msimu wa 2024/25.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.