MSHAMBULIAJI wa Simba, Steven Mukwala maarufu kama mshambuliaji mrefu kuliko goli, mipira ya juu haruki ni waa, leo Novemba Mosi amefunga bao kwa kurukia mpira wa juu.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Lake Tanganyika umesoma Mashujaa 0-1 Simba bao likifungwa na Mukwala kwa pigo la kichwa baada ya kuruka juu kuufuata mpira uliopigwa na Awesu Awesu.
Jioni kabisa kama ambavyo mtangazaji wa Azam TV, Kabombe ambaye kwa sasa anapambana kurejea kwenye ubora husema ilikuwa hivyo kwa Simba kupata ushindi huo katika mchezo dume mwanzo mwisho.
Kibu Dennis kwenye mchezo wa leo alikosa nafasi zaidi ya mbili huku Ismail Mgunda mshambuliaji wa Mashujaa akiwa mwiba kwa mabeki wa Simba wakiongozwa na Che Malone.
Simba inafikisha jumla ya pointi 22 nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 9 msimu wa 2024/25 vinara ni Yanga wenye pointi 24 baada ya kucheza mechi 8.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.