YANGA HAO NAMBA MOJA KWENYE MSIMAMO

PACOME Zouzoua anefunga bao pekee la ushindi mbele ya Singida Black Stars dakika ya 67 kwa shuti kali la mguu wa kushoto akiwa nje kidogo ya 18.

Sasa Yanga inakuwa namba moja baada ya kucheza mechi 8 mfululizo bila kufungwa ikishinda zote mazima ndani ya uwanja na pointi 24.

Singida Black Stars inashushwa kutoka namba moja mpaka mbili ikiwa na pointi 21 na mchezaji bora wa mchezo ni Pacome kutoka New Amaan Complex.

Faulo 33 jumla zimechezwa kwenye mchezo wa leo huku Singida Black Stars ikicheza jumla ya faulo 16 na Yanga 17.

Ni mchezo wa kwaza kwa Singida Black Stars kupoteza ndani ya ligi msimu wa 2024/25 ikiwa haijafanikiwa kufunga pia kwenye mchezo wa leo kwa kuwa katika mechi 8 zilizopita ilikuwa na wastani wa kufunga.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.