KIUNGO Feisal Salum amefunga bao la kwanza msimu wa 2024/25 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ken Gold uliochezwa Oktoba 25 2024 waliposepa na pointi tatu mazima kwenye mchezo huo.
Mchezo huo jumla mabao matano yalifungwa ambapo mwamuzi alikuwa Ahmed Arajiga aliamua mapigo mawili ya penalti mojamoja kwa kila timu kutokana na wachezaji kucheza faulo ndani ya 18.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Azam FC 4-1 Ken Gold. Ni pointi 18 kibindoni wanazo Azam FC nafasi ya nne na Ken Gold nafasi ya 16 ikiwa na pointi 5.
Fei alipachika bao la kwanza dakika ya 19 kwa mkwaju wa penalti Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 4-1 Ken Gold.
Katika msimamo Azam FC ni nafasi ya 4 pointi 18 baada ya mechi 9 safu ya ushambuliaji imefunga mabao 12. Mchezo ujao kwa Azam FC, ni Dar Derby dhidi ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ambapo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.