MDAKA MISHALE KARUDI, DUBE NDANI

KIPA namba moja wa Yanga, Djigui Diarra amerejea langoni hivyo ataanza mbele ya Singida Black Stars kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, New Amaan Complex kwa wababe wawili kuwa uwanjani kusaka pointi tatu.

Miguel Gamondi Kocha Mkuu wa Yanga ameanza na Dennis Nkane ikiwa ni mchezo wake wa kwanza kuanza kikosi cha kwanza, Boka, Bakari Mwamnyeto, Job, Aucho, Aziz Ki, Duke Abuya, Chama, Dube na Pacome wameanza kikosi cha kwanza.
Khomeny aliyeanza mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union, Kibabage, Bacca, Ibrahim, Sure Boy, Maxi, Mudathir, Hussein, Baleke na Mzize hawa wameanzia benchi.
Mchezo uliopita kwa Yanga ilikuwa dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na iliibuka na ushindi wa bao 1-0 waliposepa na pointi tatu na wapinzani wao Singida Black Stars walisepa na pointi tatu kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate ya Issa Mbuzi.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.