MTAMBO wa mabao Simba, Jean Ahoua bado haujawa fiti asilimia 100 kutokana na yale anayofanya kutofikia kwenye ubora mkubwa jambo ambalo linapaswa kufanyiwa kazi.
Ahoua kahusika katika mabao saba ndani ya kikosi cha Simba, akiwa amefunga mabao matatu na pasi nne za mabao, alikosekana katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, Mbeya kwa kuwa alipata maumivu Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga.
Simba ikiwa imefunga mabao 16 baada ya kucheza mechi 8 na pointi 19 kibindoni yeye anaongoza kwa wakali wa kucheka na nyavu katika kikosi cha Simba.
Mchezo ujao kwa Simba ni Novemba Mosi, Ijumaa itakuwa Uwanja wa Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma kwa kila timu kupambania pointi tatu.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa bado Ahoua hajafikia asilimia 100 za ubora wake.
“Ahoua ni kiungo mzuri ila kwa ambayo anaonyesha uwanjani bado hajafikia asilimia 100 hivyo kuna kazi inaendelea kufanyika kwake akifikia 30 atakuwa na balaa akifika 50 unadhani itakuaje?