SABABU MECHI YA SIMBA V JKT KUTOCHEZWA

OFISA Habari wa Bodi ya Ligi Tanzania, Karimu Boimanda amebainisha kuwa wamepokea taarifa kutoka uongozi wa JKT Tanzania kuhusu kupata ajali na maombi ya mechi kuahirishwa ambapo mchezo wao wa ligi dhidi ya Simba uliotarajiwa kuchezwa Oktoba 29 2024 umeahirishwa.

Boimanda amesema: “Mara nyingi huwa ninakuwepo hapa pamoja na wachezaji, manahodha kwenye eneo hili, imekuwa tofauti leo. Tumepata taarifa kuwa Klabu ya JKT Tanzania ilipata ajali hapo jana wakati ikirejea kutoka Dodoma ambapo walikuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji.

“Basi walilokuwa wamepanda lilipata ajali maeneo ya Mbweni kwa niaba ya Bodi ya Ligi Tanzania tunawaombea warejee kwenye ubora . Kwanza tumepokea barua kutoka JKT Tanzania kuhusu kuomba kuahirishiwa michezo miwili inayofuata na tumepokea barua kutoka kwa daktari wa JKT Tanzania kuhusu hali za wachezaji.

“Kwa wale ambao walipata ajali wachezaji na viongozi tunawaombea wapone haraka warejee kwenye ubora wao hivyo tulipokea taarifa kuwa wanaomba mechi zao mbili kuahirishwa ambapo mchezo wao uliokuwa unafuata ilikuwa dhidi ya Simba uliotarajiwa kuchezwa kesho.

“Mchezo mwingine ulikuwa ni dhidi ya Namungo ambao ulitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa Novemba 4 na wenyewe umeahirishwa kutokana na sababu ambazo zimetajwa. Hii ni taarifa ambayo tumeipokea hivyo mechi hizi zitapangiwa tarehe, tunawapa pole sana JKT Tanzania tukiwaombea wachezaji na viongozi waliopata ajali wapate nafuu mapema.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.