BEKI WA SIMBA ANAFIKIRIA KUFUNGA ZAIDI

BEKI wa Simba, Che Malone ana hasira na nyavu kutokana na kupania kuendelea kufunga pale anapopata nafasi ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani msimu wa 2024/25.

Ipo wazi kwamba beki huyo anashikilia rekodi ya kuwa nyota wa kwanza kufunga ndani ya ligi kwa upande wa Simba ilikuwa Uwanja wa KMC Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 3-0 Tabora United.

Bao hilo alipachika dakika ya 14 na alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo baada ya dakika 90 bao la pili alifunga kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, ilikuwa dakika ya 5 na katika mchezo huo alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.

Nyota huyo ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids hata Oktoba 19 2024 alikuwa kikosi cha kwanza kwenye Kariakoo Dabi walipopoteza kwa ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 0-1 Yanga.

“Ninapenda kuona tunapata matokeo, furaha kubwa kuendelea kushinda kwa ajili ya timu na nikipata nafasi nitaendelea kufunga kwani malengo ni kuona timu inashinda na mashabiki wanafurahi.”

Kwenye msimamo wa ligi Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 19 baada ya kucheza mechi 8 vinara wa ligi ni Singida Blacks Stars wenye pointi 22 baada ya kucheza mechi 8, Yanga ni nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 7 ikiwa imekusanya pointi 21.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.