YANGA kwenye kibarua kizito leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya Coastal Union ya Tanga.
Ipo wazi kwamba Yanga baada ya kucheza mechi 6 mfululizo haijapoteza wala kufungwa na ilicheza Kariakoo Dabi Oktoba 19 ubao wa Uwanja wa Mkapa ukasoma Simba 0-1 Yanga na mchezo uliopita ilikuwa Uwanja wa Azam Complex ubao ulisoma Yanga 2-0 JKT Tanzania.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa wanatambua ugumu uliopo kuwakabili wapinzani wao Coastal Union lakini wana amini watapata pointi tatu muhimu.
“Mchezo wetu dhidi ya Coastal Union utakuwa mgumu lakini tuna amini tutapata pointi tatu, wachezaji wapo tayari kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi.”
Yanga imekusanya pointi 18 baada ya mechi sita nafasi ya tatu ni mabingwa watetezi wa ligi huku vinara wakiwa ni Singida Black Stars wenye pointi 22 baada ya kucheza mechi 8.
Coastal Union ambayo kwa sasa ipo chini ya Kocha Mkuu, Juma Mwambusi imekusanya pointi 8 baada ya kucheza mechi nane ikiwa nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, TUNAOMBA ODA kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.