SIMBA, YANGA ZATAJWA KWENYE ORODHA YA TIMU 10 ZINAZOWANIA TUZO YA KLABU BORA MWAKA 2024

Vilabu vya Tanzania zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC, Simba Sc na Yanga Sc zimetajwa kwenye orodha ya timu 10 zinazowania tuzo ya klabu bora mwaka 2024 ya soka la wanaume iliyotangazwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

Vilabu vingine vilivyotajwa ni pamoja na Mabingwa wa Afrika msimu uliopita, Al Ahly, Mabingwa wa kombe la Shirikisho, Zamalek Fc, Mamelodi Sundowns, TP Mazembe na Petro Atletico.

Miamba wengine ni pamoja na Dreams FC, Esperance Tunis, RS Berkane, Simba Sc na Young Africans Sc.