KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Mwenge saa 10:00 jioni kuna mastaa wa Simba zaidi ya wawili ambao wataukosa mchezo huo kutokana na kutokuwa fiti.
Ikumbukwe kwamba Jean Ahoua, Yusuph Kagoma na Abdulazack Hamza ambayr ni beki hawa wote walikosekana mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Sokoine walipata maumivu kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi
Nouma pia anasumbuliwa na mafua hivyo kuna hatihati akakosekana kwenye mchezo wa leo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili ndani ya uwanja.
Oktoba 22 Simba ilipata matokeo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons baada ya dakika 90 ubao ulisoma Tanzania Prisons 0-1 Simba bao likifungwa na Che Malone ambaye ni beki.
Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amesema kuwa ripoti ya madaktari itatoa picha ya nani ambaye atakuwa tayari kwa mchezo kutokana na maendeleo yao.
“Kuna wachezaji ambao tunasubiri ripoti kutoka kwa madaktari hapo tutajua kuwa wanaweza kucheza au bado watahitaji muda zaidi, kikubwa ni kuona tunapata matokeo kwenye mchezo wetu ujao na kuwaona wachezaji wakirejea kwa mara nyingine uwanjani.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.