LIGI Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kwa mara nyingine tena mzunguko wa kwanza msimu wa 2024/25 ambapo kuna viwanja vitatu vitakuwa kwenye mtafutano wa pointi tatu.
Ikumbukwe kwamba mabingwa watetezi wa ligi ni Yanga wao watakuwa na kazi Oktoba 26 kusaka pointi tatu dhidi ya Coastal Union ya Tanga.
Oktoba 25 2025 hizi hapa mechi ambazo zinatarajiwa kuchezwa namna hii:-
Singida Black Stars ambao ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 19 baada ya kucheza mechi 7 watakuwa Uwanja wa Liti dhidi ya Fountain Gate itakuwa saa 8;00 mchana.
Simba itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Namungo FC ambao nao wanazihitaji pia pointi tatu itakuwa saa 10: 00 Uwanja wa KMC, Complex.
Azam FC watakuwa na kibarua mbele ya Ken Gold saa 1:00 usiku Uwanja wa Azam Complex.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.