FOUNTAIN GATE WATUMA UJUMBE HUU BLACK STARS

ISSA Liponda, maarufu kama Issa Mbuzi, Ofisa Habari wa Fountain Gate ameweka wazi kuwa watawanyamazisha wapinzani wao Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Oktoba 25 Fountain Gate itakuwa Uwanja wa Liti kusaka pointi tatu mbele ya Singida Black Stars unaotarajiwa kuchezwa saa 8:00 mchana na utakuwa mubashara Azam TV.

Ipo wazi kuwa Singida Black Stars ni vinara wa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi 7 wamekomba pointi 19 wakiwa hawajapoteza mchezo msimu wa 2024/25 kama ilivyo kwa mabingwa watetezi wa ligi ambao ni Yanga baada ya kucheza mechi 6.

Mbuzi amesema: “Tunajua hawajafungwa na tunajua wanafurahia kuwa namba moja sasa ni muda wa kwenda kuwanyamazisha na kuwapa huzuni wakiwa nyumbani tupo tayari na tumejiandaa kwa hili.”

Mchezo uliopita Fountain Gate ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Kwaraa ukisoma Fountain Gate 3-1 KMC, bao la kwanza kwa Fountain Gate lilifungwa kwa pigo huru dakika ya 8 na Dickson Ambundo likamshinda mlinda mlango wa KMC, Fabian Mutombola.

Fountain Gate baada ya kucheza mechi 8 imekusanya pointi 16 nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi ambayo ina ushindani mkubwa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.