LIGI KUU KUENDELEA TENA LEO, PRISONS VS SIMBA, YANGA VS JKT TANZANIA

LIGI Kuu ya soka ya NBC Tanzania bara inaendelea tena leo Oktoba 22, 2024 kwa mechi mbili ambapo Mnyama, Simba Sc atajiuliza dhidi ya Wajelajela, Tanzania Prisons saa 10:00 jioni katika dimba la Sokoine baada ya kupoteza mchezo wa derby ya Kariakoo dhidi ya watani zao, Young Africans Sc.

Katika mchezo mwingine, washindi wa derby, Yanga Sc watakuwa wenyeji wa maafande wa JKT Tanzania katika dimba la Azam Complex, Chamazi majira ya saa 1:00 usiku.

16:00 | TZ Prisons vs Simba Sc
🏟️ Sokoine, Mbeya

19:00 | Yanga Sc vs JKT Tanzania
🏟️ Azam Complex, Chamazi