DJIGUI DIARRA ANA BALAA ZITO

KIPA wa Yanga Djigui Diarra ana balaa zito uwanjani kutokana na kasi yake ya kuokoa hatari ndani ya lango akicheza mechi tano mfululizo bila kufungwa.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 Diarra alipishana na tuzo ya kipa bora ambayo ilikwenda mikononi mwa Ley Matampi ambaye msimu wa 2024/25 akiwa na Coastal Union hajawa katika ubora wake kwa kuwa amekuwa akifungwa kwenye mechi ambazo anaanza kikosi cha kwanza.

Rejea mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC, baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-2 Coastal Union ambapo Matampi alifanya kosa moja kwenye kuokoa hatari bao likafungwa na Mohamed Hussen mwisho waligawana pointi mojamoja kwenye mchezo huo.

Diarra ameanza langoni mechi zote tano za Yanga ambapo hawajafungwa zaidi ya kushuhudia timu hiyo ikishinda mfululizo na kukomba pointi 15 mazima ndani ya ligi.

Haya hapa matokeo ya mechi ambazo Diarra alianza kikosi cha kwanza chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi namna hii:-

Kagera Sugar 0-2 Yanga mchezo huu ulichezwa Uwanja wa Kaitaba, Agosti 29 2024 na mtupiaji wa bao la kwanza ni Maxi Nzengeli ndani ya Yanga kwenye ligi.

Ken Gold 0-1 Yanga huu ulikuwa mchezo wa pili kwa Yanga ugenini ilikuwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya mtupiaji alikuwa ni Ibrahim Bacca ambaye alitumia pasi ya Aziz Ki Septemba 25 2024.
Yanga 1-0 KMC, mchezo wa kwanza wakiwa Uwanja wa Azam Complex msimu wa 2024/25 ilikuwa Septemba 29 2024.

Yanga 4-0 Pamba Jiji ushindi mkubwa kwa Yanga ndani ya 2024/25 walikuwa Azam Complex  ilikuwa Oktoba 3 2024.

Oktoba 14 2024, Simba 0-1 Yanga mchezo wa kwanza kupoteza mtupiaji ni Maxi Nzengeli dakika ya 86. Leo Oktoba 22 Yanga itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Azam Complex.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.