CHE MALONE APELEKA KILIO KWA WAJELAJELA

WAJELAJELA Tanzania Prisons wamepoteza mchezo wakiwa nyumbani mzunguko wa kwanza mbele ya Simba baada ya dakika 90 kukamilika.

Bao pekee la ushindi limefungwa dakika ya 5 na Che Malone baada ya Mussa Mbisa kutema faulo akiwa ndani ya 18 iliyopigwa na Kibu Dennis.
Baada ya bao hilo Prisons waliongeza umakini na kuongeza ulinzi hasa wakimzuia mshambuliaji Leonal Ateba ambaye alikwama kukomba dakika 90 nafasi yake ilichukuliwa na Mukwala ambaye alifanya jaribio moja ambalo liliokolewa na Mussa Mbisa.

Shomari Kapombe alipewa majukumu ya kurusha mipira na kupiga krosi huku Fabrince Ngoma akiwahimiza wachezaji wa Simba kila wakati pale wanapopoteza mpira.

Doto Shaban nyota wa Tanzania Prisons utulivu mkubwa kweye uwanja na jaribio lake la dakika ya 86 kidogo litibue shughuli kwa Simba licha ya nyota huyo kuonyeshwa kadi ya njano dakika ya 75.

Simba inafikisha pointi 15 baada ya kucheza mechi 7 mchezo wao uliopita ilipoteza kwenye Kariakoo Dabi kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.